September 27, 2021

 


BARBARA Gonzalez, Mtendaji Mkuu wa Simba, ameweka wazi kuwa wanakwenda kuanza msimu mpya wa 2021/22 kwa mambo mapya jambo ambalo litakuwa ni rekodi kwa timu hiyo.

Akizungumza na Spoti Xtra, Barbara alisema kuwa wanatambua juu ya umuhimu wa mechi zao za ligi pamoja na mipango iliyopo, hivyo watakuwa tofauti katika kila jambo.

“Nadhani ni msimu mpya, hapo sisi tunapaswa kuwa na mambo mapya, kwetu kila kitu ni kipya, kuanzia mbinu, wachezaji wetu nao wana mipango mipya.

“Jambo la msingi kwa sasa ni mashabiki kuendelea kuwa nasi bega kwa bega kwani Simba ni timu kubwa, hivyo inahitaji kuwa na matokeo makubwa pia katika yale ambayo yanafanyika,” alisema Barbara.


Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Biashara United ya Mara kwenye mchezo wa kwanza wa ligi.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Septemba 28, Uwanja wa Karume, Mara.

2 COMMENTS:

  1. Tupo pamoja kulisongesha. Ila chonde chonde kocha atumie vijana akina Kibu Dennis, Muhilu, Sakho, Kanute na wengineo waoneshe ubora wao

    ReplyDelete
  2. Hakika tupo pamoja mabingwa wa nchi simbasc hakuna kukata tamaa tujipange zaidi kwaajili ya kulitetea kombe letu la ligi kuu na Fa cup.
    Barbara wewe ni superwoman tuna imani na utendendaji wako ktk maendeleo na maslahi ya simbasc Mungu akubariki sana uwe imara zaidi hatutingishwi na Msukule.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic