September 27, 2021

 


LEO Septemba 27, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza kikosi cha timu ya taifa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Benin.


Mchezo huo ni kwa ajili ya kufuzu Kombe la Dunia na umejumuisha wachezaji hawa:-

Aishi Manula, (Simba) Metacha Mnata, (Polisi Tanzania) Wilbol Maseke, (Azam FC) na Ramadhan Kabwili, (Yanga) kwa upande wa makipa.


Shomari Kapombe, (Simba), Bakari Mwamnyeto, (Yanga), Israel Mwenda, (Simba),Erasto Nyoni, (Simba),Dickosn Job, (Yanga)

Keneddy Juma, (Simba), Lusajo Mwaikenda, (Azam FC), Mohamed Hussein, (Simba), Edward Manyama, (Azam FC), Nickson Kibabage, (KMC).


Mastaa wengine ni Meshack Mwamita, (Kagera Sugar) Novatus Dismas, (Maccabi Tel Aviv ya Israel)

Mzamiru Yassin, (Simba) Jonas Mkude,(Simba) Feisal Salum, (Yanga), John Bocco, (Simba) Idd Seleman, (Azam FC) Abdul Hamis Suleiman, (Coastal Union).


Yupo nahodha Mbwana Samatta, (Royal Antwerp-Ubelgiji) Reliant Lusajo, (Namungo) pamoja na Simon Msuva, (Wydad Casablanca).


Imeandikwa na Dizo Click


4 COMMENTS:

  1. Mpira was bongo hivi makocha wanachagua wenyewe au wanachagua maana Mkude hajacheza mechi yoyote lakini kaitwa,Kibwana Shomary Pamoja na kazi yote juzi hayumo? Thomas Ulimwengu yupo wapi?Himid Mao Misri anaanza First eleven lakini hajaitwa,Mpira wetu utapona siku Yesu Kristo akija,Muzamiru na Erasto Nyoni Simba wanakaa bench lakini wanaitwa,kweli Mzee Mwinyi alisema Tanzania Kichwa Cha Mwendazimu,ukiangalia hata Kabwili sababu za kumwita hazipo,bora angeitwa Kisubi au Daniel Mgore,tuna kazi ya kufikia Cameroon,Nigeria,Misri,Ghana au Morocco,Algeria,Tunisia au Ivory Coast kwa upuuzi huu

    ReplyDelete
  2. West Africa na Africa ya Kaskazini hawana upuuzi kwenye mpira na ndiyo maana wataendelea ku dominate mpira wa Africa.Bongo Kila mtu anachagua wachezaji baada ya kuliachia bench la ufundi na kocha,Mungu tunaomba uuponye mpira wetu maana ukiangalia wengine walioitwa kwenye squad ni kichefuchefu na hata sijui kama team ya taifa Ina criteria za kuita wachezaji

    ReplyDelete
  3. Bongo kila mtu kocha. Nani alisema kila anaecheza first eleven aitwe kucheza timu ya taiga, first 11 ni game plan na mfumo wa timu sio kuwa huyo mchezaji ni mzuri sana kushinda wenzake. Makambo juzi kukaa bench alikuwa kashuka kiwango au?. Muacheni mwalimu afanye kazi, kochi ni mmoja

    ReplyDelete
  4. Kagere anaitwa rwanda kila siku kwani hawajui kuwa anakaa bench ila kwenye mfumo wa timu yao anafaa, juko moshid alikuwa anakaa bench simba ila Uganda anaitwa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic