UKIWEKA kando vita ya kusaka pointi za kutosha ndani ya Ligi Kuu Bara ili timu kuweza kusaka ubingwa pia vita nyingine ambayo ilikuwa inafukuta kwene timu zilizo ndani ya tatu bora ni ile ya kutupia mabao mengi na mabingwa walikuwa Simba waliosepa na ubingwa pia wa ligi.
Katika mechi
34 ambazo ni dakika 3,060 Simba ilifunga jumla ya mabao 78 ikiwa na wastani wa
kucheka na nyavu kila baada ya dakika 39.
Mbali na
Simba kuwa namba moja kwa utupiaji na mfungaji bora kwa msimu wa 2020/21
alitoka kwenye kikosi hicho ambacho kinanolewa na Didier Gomes raia wa Ufaransa
akishirikiana na mzawa Seleman Matola.
Alikuwa John
Bocco ambaye naye ni mzawa alifunga jumla ya mabao 16 na alitoa pasi mbili
hivyo alihusika kwenye jumla ya mabao 18 kati ya 78 ambayo yalifungwa na timu
hiyo.
Hata
mtengeneza mipango namba moja kwa msimu wa 2020/21 alikuwa anatoka ndani ya
Simba ni Clatous Chama raia wa Zambia alifunga mabao 8 na pasi 15 lakini msimu
ujao hatakuwa ndani ya kikosi hicho kwa kuwa amesajiliwa na RS Berkane ya
Morocco.
Namba mbili
ipo mikononi mwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa
Tunisia na ilimaliza pia ligi ikiwa nafasi ya pili na safu yake ya ushambuliaji
ilifgunga jumla ya mabao 52.
Ilikuwa na
wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 58 kwenye ligi na kinara wa
mabao alikuwa ni Yacouba Songne ambaye alifunga mabao 8 pia alitoa pasi sita za
mabao.
Alihusika
kwenye jumla ya mabao 14 yaliyofungwa na timu hiyo ambayo yalimfanya awe ni
namba moja kwa utupiaji ndani ya kikosi hicho kwa msimu uliopita.
Namba tatu
ipo mikononi mwa Azam FC ambapo safu yao ilitupia jumla ya mabao 50 kibindoni
ikiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 61.
Ni Prince
Dube yeye alikuwa namba moja kwa utupiaji na alifunga mabao 14 na kutoa pasi
tano za mabao hivyo alihusika kwenye mabao 19 yaliyofungwa na timu hiyo
inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina.
0 COMMENTS:
Post a Comment