MABINGWA wa taji la Kuu Bara mara 27 ndani ya ardhi ya Tanzania Yanga wameendelea kujiweka sawa kwa ajili ya msimu wa 2021/22 licha ya baadhi ya nyota wa timu hiyo kuwa katika majukumu katika timu zao za taifa.
Mataifa mengi ya Afrika kwa sasa ni maandalizi kuelekea katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia jambo ambalo limefanya idadi ya wachezaji katika timu kupungua.
Miongoni mwa wachezaji wa Yanga walioitwa katika timu zao za taifa ni pamoja na Khalid Aucho, raia wa Uganda pia yupo Ramadhani Kabwili, Feisal Salum na Dickson Job hawa ni wazawa.
Ambao wameendelea na mazoezi miongoni mwao ni pamoja na Dickson Ambundo ambaye, Deus Kaseke, Paul Godfrey wengi hupenda kumuita Boxer.
Kwa msimu wa 2020/21, Yanga ilimaliza ikiwa nafasi ya pili baada ya kukusanya pointi 74 na ilipachika mabao 52 katika mechi 34.
Iliweka kambi kwa muda mfupi nchini Morocco kisha ghafla ikarejea ndani ya ardhi ya Tanzania na kwa sasa imeweka kambi Avic Town, Kigamboni.
0 COMMENTS:
Post a Comment