BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Mfume Mfaume amepinga vikali kauli ya Hassan Mwakinyo ya kujiita yeye ni Professional Boxer na wengine kuwa mabondia wakawaida jambo ambalo halina ukweli wowote ikiwa wote wanacheza ngumi za kulipwa.
Mfaume ametoa kauli hiyo kufuatia kauli iliyotolewa na Mwakinyo baada kuulizwa juu ya kupigana na Twaha Kiduku ambapo alijibu kwa sasa yeye anafanya Proffesional Boxing tofauti na bondia Twaha Kiduku pamoja na mabondia wengine.
Mfaume amesema:- “Mabondia wanaocheza ngumi za kulipwa nchini wote ni kama watoto wa mama mmoja hivyo wote ni Professional Boxers haijalishi bondia huyo amecheza sana na mabondia kutoka nje ya nchi au ndani ilimradi bondia huyo awe ametoka kwenye ngumi za ridhaa na kuingia kwenye ngumi za kulipwa.
“Lakini ninanatarajia pia kupanda ulingoni Octoba 30, mwaka huu na pambano hilo ambalo limeandaliwa na Kepteni Seleman Semunyu, nimeanza maandalizi nikiwa kama bondia wa kulipwa,” alisema Mfaume.
0 COMMENTS:
Post a Comment