September 19, 2021


 WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga wamepewa mbinu za kuweza kupindua meza kibabe nchini Nigeria na nyota wa zamani wa timu hiyo Mohamed Hussein, ‘Mmachinga’.


Leo Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi, ina kibarua kizito cha kusaka ushindi mbele ya Rivers United nchini Nigeria ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza Uwanja wa Mkapa kwa kufungwa bao 1-0.

Uzito wa mchezo wa leo upo katika ishu ya kupata ushindi wa mabao zaidi ya mawili na kuweza kuhakikisha kwamba ukuta wao hauruhusu bao ndani ya dakika 90 za machozi na jasho.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mmachinga alisema kuwa kwenye ulimwengu wa mpira kila kitu kinawezekana ikiwa wachezaji wa Yanga wataamua kufuata maelekezo ya benchi la ufundi na kucheza kwa kujiamini bila kukata tamaa.


“Kwa namna ulimwengu wa mpira ulivyo sasa kila kitu kinawezekana hata kupata matokeo ugenini inawezekana kwa kuwa wao waliweza kushinda kwetu basi kuna nafasi ya kwenda kushinda kwao pia.


“Kikubwa ambacho Yanga wanapaswa kufanya ni kuwa na nidhamu na kucheza kwa kufuata maelekezo ya benchi la ufundi, wachezaji wanajukumu la kufanya hivyo na inawezekana wakawapa furaha mashabiki na Tanzania kiujumla.

"Ni suala ambalo lipo kwenye uwezo wao na inawezekana. Mpira una njia na unahitaji nidhamu hivyo wawakilishi wetu bado wana nafasi ya kufanya vizuri” alisema Mmachinga. 


 

3 COMMENTS:

  1. Tunaomba kila la kheril

    ReplyDelete
  2. Mungu wet mwenye nguvu atatufanikishia, leo ushindi upo na tutasonga mbele.

    ReplyDelete
  3. Mpigwe ili mkone kushangilia wageni.Mliwapa nyoka unga leo mnalalamika kwanini wanataka kuwauma.Pigweni pumbu za kutosha.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic