October 11, 2021


 BAADA ya Azam kutoa tamko la 
kuwasimamisha mastaa wao wakongwe, Mudathir Yahaya, Abdallah Salumu ‘Sureboy’ na nahodha mkuu Aggrey Morris, hatimaye kilicho nyuma ya pazia kimefichuka.


Kutokana na taarifa waliyoitoa Azam kupitia ukurasa wao wa Instagram ni kwamba wachezaji hao wamesimamishwa kwa muda usiojulikana kutokana na kumtolea maneno yasiyo ya staha meneja wa timu, Luckson Kakolaki.


Kikizungumza na Championi Ijumaa, chanzo cha karibu cha Azam kimesema: “Ipo hivi, huwa tukishinda kila mechi kubwa za Simba, Yanga na mechi za kimataifa huwa tunapewa bonasi ya dola elfu moja (Sh 2,297,010) kila mchezaji na benchi la ufundi.


“Kabla ya mchezo wa marudiano na Horseed makapteini hao walimfuata meneja na kuwa kama wanafanya masihara kwa kusema kuwa hela itakapotoka hawatampa mtu yeyote zaidi ya wao wachezaji, maana wao ndio wanaopambana.

“Baada ya mchezo walipopewa zile hela kweli wakaenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na kuanza kugawana wenyewe bila kiongozi yeyote kuwepo.

“Baada ya siku hiyo mwalimu na viongozi wengine wakaanza kuuliza kuhusu hela ya bonasi, ndipo tukakaa kikao na walipoulizwa wakasema hela ni yao na sio ya watu wengine.


“Viongozi waliotoa hela walipoulizwa walisema hela ni ya timu nzima ndipo wakawasimamisha kwanza kabla ya kujadiliwa.


“Ilikuwa wafukuzwe kabisa ila waliona mlolongo ni mrefu sana ndiyo maana wakaamua kuwasimamisha. Na kwa muda waliosimamishwa wataendelea kulipwa mishahara na mwenye mkopo ataendelea kukatwa.”

6 COMMENTS:

  1. Kwa hiyo hasara ya issue hii iko upande upi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ukiangalia sana hasara bila ya kuzingatia matokeo ya baadae ya utovu wa nidhamu utajikuta unavuna zaidi ya hasara....."anguko la jumla la taasisi" kazi na nidhamu

      Delete
    2. Hueleweki ulichokiandika ndugu yangu

      Delete
    3. Huwezi kuelewa kwa sababu uwezo wako wa kuelewa ni mdogo,ungekuwa una angalau hata chembe ya elimu ya ufanisi wa biashara ungeelewa maana ya nilichokiandika,labada kwa kukusadia tu,nidhamu ni sehemu ndogo tu ya moja ya kanuni ya ufanisi wa kukuza biashara.Wenye weledi wamenielewa nimemaanisha nini.

      Delete
  2. HUO NI UONEVU MKUBWA SANA!
    WACHEZAJI HAWAKUKOSEA KUGAWANA MAANA NDIO WANAOCHEZA NA KUUMIA viongozi WAWE NA HEKIMA WASUBILIE MISHAHARA

    ReplyDelete
  3. Timu INAWEZA KUCHEZA Na kuwa BINGWA KWASABABU YA WACHEZAJI NA VIONGOZI WASIWEPO.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic