October 2, 2021

 


ALIYEWAHI kuwa Ofisa Habari wa Simba, Haji 
Manara, ambaye kwa sasa ni msemaji wa Yanga, amemtaka kiungo wa Simba, Bernard Morrison amjibu kuhusu suala la Mohamed Dewji kujiuzulu nafasi ya uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi.


Manara amemtaka Morrison amjibu baada ya mchezaji huyo kuwa na tabia ya kujibu kwenye mtandao wa Instagram wa Manara.

Manara ameibua hoja hiyo baada ya bilionea Mo Dewji kujiuzulu kwenye nafasi yake ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba na kubaki kama muwekezaji.



Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara amemuuliza hivi Bernard Morrison; “Bernard nimemisi kuona ukinijibu kwenye akaunti yangu, hebu niambie kipi kimemfanya Muhamedi kujiuzulu au ni zile bilioni mbili wanazomuuliza aliziweka kwenye akaunti gani ya benki ndio maana kajiuzulu maana hapendi kuulizwa.”

Morrison naye akamjibu hivi Manara;“Kuna msitari kwenye Biblia unasema kuwa nabii huwa haheshimiki kwao, kwa hiyo sijashtuka kuona unahangaika kuzidi kuipaka matope heshima ya Mohamedi

“Tafuta kampuni yoyote ya kwako au hata mwambie Injinia Hersi Said akusaidie angalau uwe na kampuni maeneo ya Mikocheni ili walau ukae kwenye levo za Mohamedi, natamani kucheka ila imoji hazitembei.”


11 COMMENTS:

  1. Manara aneshajishushia hata ile heshima kidogo aliyokuwa nayo, watu wanamhurumia tuu

    ReplyDelete
  2. Katika wajinga Manara ni kinara wao.Jambo halimhusu amevalia njuga.Simba wameshakutema bakia huko huko.

    ReplyDelete
  3. Na jamaa wanaona wamempata wa kuipa mafanikiotimu

    ReplyDelete
  4. Mjinga ni yule anaejifanya anajua kumbe kiazi. Manara anaupiga mwingi mpaka kawachanganya MO sports

    ReplyDelete
  5. Aliye kaa kimyaa ndio mwerevu,wengine wote wajinga akiwemo MANARA na wewe unaebishana hapa.na ukitaka kuona ujinga wako lazoma utatoa povu kama sabun ya unga.

    ReplyDelete
  6. Manara yupo sahihi..Mtu kama Morrison hakutakiwa kujiingiza kwenye migogoro ya kimtandao, yeye ni professional prayer aangalie mstakabali wa mpira tu..kujibizana na watu nje ya dimba naona hakumstahili km mchezaji wa kimataifa!acheze mpira.

    ReplyDelete
  7. Uyo manala yupo saikwako Leo sio sisi simba

    ReplyDelete
  8. Uyo manala yupo saikwako Leo sio sisi simba na kama kweli piya yupo said mfungulie ofisi basi

    ReplyDelete
  9. Heheheee manara anaupiga mwingi

    ReplyDelete
  10. Morrison ana akilu Sana majibu yake Yana mafundisho Sana. Inabidi Manara ajifunze kitu hapo aachane na Mo huyo sio saizi yake Ni mtu aliyemuinua ktika ulimwengu wa soka.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi kesi ya Morrison Na YANGA niaje jamani ???

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic