October 12, 2021


 NYOTA wa timu ya taifa, Neymar Jr ameweka wazi kwamba baada ya kucheza Kombe la Dunia lijalo la mwaka 2022 hajui kama akili yake itakuwa tayari kuendelea kupambana kwenye soka au laa.

Kauli hiyo inaamanisha kwamba huenda baada ya kukamilika kwa Kombe la Dunia linalotarajiwa kufanyika nchini Qatar staa huyo anaweza kustaafu masuala ya mpira.

Brazil kwa sasa inapambania tiketi ya kuweza kufuzu Kombe la Dunia na nyota huyo anayekipiga ndani ya Klabu ya PSG aliweza pia kuwa kwenye kikosi kilichonyooshwa mabao 7-0 dhidi ya Ujerumani kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Dunia.

Staa huyo amesema kuwa kombe la dunia la mwakani ndilo litakuwa la mwisho kwake kucheza kwa sababu hajui baada ya hapo atakuwa tayari kuendelea kucheza.

"Nafikiri Kombe la Dunia lijalo litakuwa la mwisho kwangu, nahisi itakuwa hivyo kwa sababu sijui kama nitakuwa tayari kuendelea kucheza na sijui akili yangu itakuwa tayari kuendelea kupambana ama laa," .



3 COMMENTS:

  1. Habari za Naimar sawa ila nilidhani ingekuwa busara kuwazungumzia akina Yusufu Muhilu na David Bryson wa Yanga na Wachezaji kadhaa ambao wakifanyiwa scouting nzuri ya kuwaingiza kwenye Taifa Stars watakuwa ni msaada kutokana kuwa na maumbo ya kugongana na wa Benini vizuri.Serious muda huu waandishi wetu jitahidini Sana kutoa mawazo ya kuijaza nyama Taifa Stars ili iwe Bora zaidi kuliko kupoteza muda kuleta story isiokuwa na faida. Wabrazili wana akina Naimar chungu tele hata asipokuwepo Brazil itabaki kuwa Brazil kwenye soka.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakuunga mkono kabisa, habari za nchi nyingine za nini?kwani zinatuhusu?

      Delete
  2. Mwandish ww Muongo,brazil walipo fungwa saba neymar alikuwa hayumo ni Injury 😁usitudanganye

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic