October 6, 2021

 


NYOTA ya Mohamed Salah raia wa Misri anayekipiga ndani ya Liverpool inatajwa kuwa kali kwa kuwa katika mechi zote ambazo amecheza mpaka sasa hajawahi kuonja joto ya kadi nyekundu akiwa amecheza jumla ya mechi 165.

Kwenye mechi hizo ambazo amecheza ni kadi za njano tano amekusanya kwa kuonyeshwa kutokana na kuwachezea wachezaji wenzake faulo.

Rekodi zinaonyesha kwamba Salah amecheza jumla ya faulo 87 na katika ishu ya kuotea ili aweze kufunga mabao amefanya hivyo mara 83.

Anatajwa kuwa mlinzi licha ya kuwa mshambuliaji kwa kuwa aliweza kuzuia jumla ya mashuti 149 yaliyokuwa yanakwenda kwenye lango lao na aliweza kuivuruga  mipira 28 iliyokuwa kwa wapinzani wao.

Pia kwa vichwa nyota huyo si haba akiwa karibu na lango lake kwani aliweza kupiga jumla ya vichwa 12 katika harakati za kuzuia mipira isiingie kwenye nyavu za lango lake.

Nyota huyo ni wa kwanza kufunga mabao zaidi ya 20 kwa misimu mitatu tofauti ya Ligi Kuu England jambo ambalo ni rekodi kwake ndani ya Liverpool.

Ilikuwa ni msimu wa 2017/18,2018/19 na 2020/21 aliweza kufunga mabao zaidi ya 20 na aliwahi kufunga mabao 32 msimu wa 2017/18 na kuvunja rekodi ya Cristiano Ronaldo aliyefunga mabao 31 msimu wa 2007/2008. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic