October 4, 2021


 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa walianza kwa kusuasua kwenye Ligi Kuu Bara kwa kuwa walikuwa bado hawajajua ligi itakuwa ya aina gani kwa msimu wa 2021/22.

Tayari mabingwa hao watetezi wa taji la Ligi Kuu Bara wameambulia ushindi mmoja kwenye mchezo wa ligi na walitoshana nguvu na Biashara United kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Karume, Mara.

Gomes amebainisha kwamba kwenye mchezo wa kwanza walipata shida kuweza kushinda kwa kuwa walikuwa bado hawajajua aina ya ligi itakavyokwenda.

"Tulianza kwa shida msimu huu kwa kuwa hatukujua ligi inakwendaje na hilo limetufanya tuweze kujua namna gani tunaweza kwenda hiloawali lilitufanya tukashindwa kupata ushindi mchezo wetu wa kwanza mbele ya Biashara United.

"Kwa sasa tumejua aina ya ligi ilivyo na mtindo ambao unahitajika tutakwenda sawa na imani yetu ni kuona kwamba tunapata matokeo chanya kwenye mechi zetu ambazo tutacheza," amesema.

Katika mchezo wa kwanza kushinda ilikuwa ni mbele ya Dodoma Jiji na ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri,Dodoma.

9 COMMENTS:

  1. Sasa kama Simba kaanza kwa kusuasua Azam kaanza kwa nini? Yaani Simba hajapoteza mchezo wowote halafu kaanza kwa kusuasua mechi zenyewe zilizochezwa mpaka sasa ni mbili peke yake. Utakataka kwenye uandishi wa hovyo kumlishia maneno kocha asioyasema ni moja Kati ya mambo yanayoondosha ladha katika tasnia ya uandishi wa michezo nchini. Kiukweli Simba ameanza ligi vizuri tena Sana hasa ukichukulia Simba ameanzia mechi zake ugenini kwenye viwanja ghasi vilivojaa kila aina ya fitina na bado Simba ameondoka na point kadhaa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. AZAM IMEANZA KWA KUCHECHEMEA.
      Kama wewe HUPENDI kilichoandikwa Na wengine ndivyo ilivyo Na ulichokiandika .

      SIMBA ingeanza vizuri ingeanza Na USHINDI wa goli nyingi bila kujali Ni ugenini kwasababu usajili wa SIMBA sisawa Na Biashara kwa gharama Na malengo.pia si sawa Na Dodoma city .


      SIMBA imekuwa Na UIMARA KUANZIA MASHABIKI NI BORA ,GOLIKIPA BORA,VIUNGO BORA NA WASHAMBULIAJI BORA!
      BY KOMANDOO

      Delete
    2. Huyo anayempinga mwandishi hajielewi, Simba ndio bingwa na alitakiwa kuanzia kibingwa.. sasa kwa nini asiseme imesuasua? Draw..halafu ushindi mwembamba dhidi ya timu iliyocheza pungufu!

      Delete
    3. UBINGWA wa mwaka Jana sio sawa Na Mwaka huu Na usajili haufanani hata Biashara ya Mwaka Jana si sawa Na hii ya Mwaka huu hilo halihitaji Shule Ni uelewa Na Ufahamu.

      Delete
    4. Sasa hiyo miaka minne ilikuwaje? So haifanani na bado akaendelea kuwa bingwa na huo ni mfano hai hauhitaji data za kutengeneza!

      Delete
  2. Eti mtu anakazana kusema kuwa ushindi mwembamba dhidi ya timu iliyocheza pungufu,hakuna timu iliyoingia uwanjani pungufu,ni matokeo ya mchezo mbaya ulioufanya wachezaji wa Simba watolewe nje Kwa kuumizwa na kufanya kocha kufanya sub za lazima.Kwa hiyo usikazanie kusema Simba imecheza na timu iliyokua na wachezaji pungufu.Vitendo vilivyofanywa na wachezaji wa Dodoma Jiji vilivyowapelekea kucheza pungufu Kwa namna nyingine ndivyo viliifanya Simba isishinde magori mengi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pungufu ni pungufu tu, wachezaji 10 sio sawa na 11.

      Delete
  3. Simba hatukuanza vzr Huo ndo Ukweli,,Ila tuna matumaini Tunaenda kufanya vizuri

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic