October 4, 2021


FEISAL
 Salum ‘Fei Toto’, amesema hawatakuwa tayari kuona wanapoteza mchezo wowote katika ligi misimu huu, ukiwemo dhidi ya Simba, kwa kuwa anaamini wana kikosi bora tofauti na wapinzani wao.


Kiungo huyo ametoa kauli hiyo kufuatia kufanikiwa kufunga bao pekee katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera na Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mfungaji wa bao la kwanza kwa Yanga ni Fei ambaye aliweza kuipa pointi tatu timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Fei Toto alisema kuwa imekuwa ni furaha kubwa kwake kufunga bao la kwanza katika msimu huu kwa timu yake, hali ambayo anaamini itaongeza hali ya kupambana kwa timu nzima kwa kuwa hawatakuwa tayari kupoteza mchezo wowote msimu huu.


“Kwanza, kwangu imekuwa furaha ya kuweza kufunga bao la kwanza kwa timu yangu msimu huu, hii ni hatua nzuri kwa sababu tupo hapa kwa ajili ya kufikisha malengo ya timu kuona tunapata matokeo katika kila mchezo.


“Ligi ni ngumu kwa kuwa kila timu imejiandaa kupata matokeo.Wapinzani wetu nao wanahitaji matokeo mazuri lakini bahati imekuwa upande wetu tumeshinda maana naamini hatutakuwa tayari kuona tunapoteza mchezo wowote msimu huu ili kuweza kufikia malengo,” alisema Fei Toto.

Mchezo wa pili wa Yanga ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold na kuweza kufikisha jumla ya pointi sita kibindoni.

7 COMMENTS:

  1. Hata Man city huwa wanafungwa, jana Bayern kachezea kichapo, sembuse huo utopolo wa yanga usifungwe wao nani? Mpira haiendi hivyo ndio kaana wakifungwa lazima wapate mtu wa kulaumu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kila timu ina malengo yake, infante jitihada za kuyatimiza, sasa povu la nini?

      Delete
    2. Usiwe mpumbavu hakuna timu ambayo ina plan kufungwa ikitokea inakuwa bahati mbaya tu

      Delete
  2. Timu hadi leo inaendeshwa kishirikina, kila mechi lazima waparamie ukuta au wavunje mageti ili kusaka ushindi kichawi hata aibu hakuna?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Je yale mapaka yetu haukuwa ushirikina???

      Delete
    2. Acha mambo ya kijinga jinga we kolo. Kila timu ina mikakati na siku zote kuwania ubingwa lazma kila mechi iwe fainali. Sasa wewe unataka tuwaachie kikombe. Huu msimu tuna wabana in and out of the ground

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic