October 8, 2021

 


WACHEZAJI wa timu ya Tanzania, Taifa Stars wakiwa katika ndege ya Air Tanzania aina ya Airbus A220-300 tayari kwa safari ya Benin ambayo itachukua saa 5:20.

Stars inayonolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen ina kibarua cha kwenda kusaka pointi tatu mbele ya Benin kwa ajili ya kuwania tiketi ya kucheza Kombe la Dunia Qatar 2022.

Katika mchezo uliochezwa jana Oktoba 7, Stars ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 hivyo ina kibarua kizito cha kusaka ushindi ugenini.

Poulsen amesema kuwa anawaamini vijana wake wanaweza kupata matokeo kwenye mchezo huo kwa kuwa makosa ambayo wameyafanya watayafanyia kazi.

"Makosa ambayo tumeyafanya kwenye mchezo wa mwanzo tutayafanyia kazi ili kuweza kupata ushindi kwenye mchezo wetu wa marudio.

"Vijana walikuwa wanahitaji ushindi ila walikwama kumalizia nafasi ambazo walitengeneza hivyo bado tuna muda wa kufanya kwenye mechi ijayo," .

3 COMMENTS:

  1. Yani kwenye taarifa kama hii unakosa kuandika kuwa mechi hiyo ya marudiano inachezwa lini?

    ReplyDelete
  2. Plot 89 block 25 makao makuu majengo defense kwa Benin kuwahi ni professional tofauti mfungaji wa Benin kuwahi tu penye professional live

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic