MSHAMBULIAJI wa Yanga, Heritier Makambo raia DR Congo, amefunguka kuwa matarajio yake ni kuona msimu huu wanafanikiwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara mbele ya wapinzani wao Simba kwa kuwa wao wana kikosi imara na kina uwezo wa kupata matokeo kwenye mchezo wowote ukiwemo wa wapinzani wao, Simba.
Makambo ni moja ya wachezaji ambao wamesajiliwa na Yanga kwa ajili ya kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho msimu huu wa ligi ikiwa ni baada ya timu hiyo kukaa misimu minne bila kutwaa ubingwa.
Yanga wameanza na kasi ya kushinda mechi zao mbili za ligi wakiwa na pointi sita zikiwa mbili mbele ya Simba ambao wenyewe wameshinda moja na sare moja.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Makambo alisema kuwa malengo yake msimu huu ni kuona Yanga inafanikiwa kutwaa ubingwa mbele ya wapinzani wao Simba kutokana na ubora wa kikosi chao kwa kuhakikisha wanapata matokeo bora katika kila mchezo.
“Jambo kubwa ambalo lipo kwangu ni kuona naipambania timu kuweza kupata matokeo maana tunataka ubingwa wa msimu huu. Nataka kuisaidia timu kupata matokeo ikiwemo suala la kufunga mabao ndiyo kipaumbele kikubwa lakini kuona tunashinda kila mchezo kutokana na ubora wa timu yetu.
“Tumewafunga Simba kwenye ngao lakini tunahitaji kuifunga pia kwenye ligi ili tuweze kufikia tunapotaka kwa kuweza kushinda kila mechi,” alisema Makambo.
Makambo cheza mpora punguza maneno
ReplyDeleteKwani mpaka sasa yeye mwenyewe keshatia magoli mangapi?
ReplyDeleteSimba haiwezi kufungwa na yanga mara mbili mfululizo na yanga haiwezi kufungwa na simba mara mbili mfululizo
ReplyDeleteFact
Delete