KOCHA Mkuu wa Klabu ya DTB inayoshiriki Championship, Ramadhan Nswazurimo amesema kuwa ushindi ambao wameupata leo kwenye mchezo wao dhidi ya African Lyon ni jambo la furaha kwao na anautoa zawadi kwa mwanaye ambaye leo ni kumbukizi yake ya kuzaliwa.
Aidha ameongeza kuwa mchezaji wake Amiss Tambwe ambaye amefunga mabao yote wakati ubao wa Uwanja wa Uhuru ukisoma DTB 4-1 African Lyon alikuwa na nafasi ya kufunga mabao sita na anaamini anaweza kuwa mfungaji bora hapo baadaye.
0 COMMENTS:
Post a Comment