October 13, 2021


 KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amepanga kwamba, baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC utakaochezwa Oktoba 19, mwaka huu, atatumia takribani siku tisa kukijenga kikosi chake kuimaliza Azam FC.

Katika maandalizi hayo ya siku tisa kuiwinda Azam, Yanga inatarajiwa kucheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya timu kutoka Kenya kati ya Sofapaka au Tusker.


Kabla ya hapo, Jumapili, Yanga ikicheza mechi ya kirafiki dhidi ya JKU ya Zanzibar kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Katika mchezo huo Yanga ilishinda bao 1-0 na mtupiaji alikuwa ni Fiston Mayele ambaye alipachika bao hilo kipindi cha kwanza lilidumu mpaka dakika 90 zilipokamilika.


 Chanzo kutoka ndani ya Yanga, kimeliambia Spoti Xtra kuwa: “Kocha Nabi hataki masihara kabisa na timu yake kwani baada ya mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, aliomba siku 30 kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake cha msimu huu.

“Kwa sasa ndicho anachokifanya kwani baada ya timu kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya JKU ya Zanzibar, hesabu ni kuelekea mkoani Songea kwenye mechi dhidi ya KMC.

“Baada ya mchezo dhidi ya KMC timu itaelekea moja kwa moja Arusha ambapo timu itaweka kambi ambayo itakuwa ya takriban siku tisa.

“Wakiwa huko watacheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya timu ya Kenya kati ya Sofapaka au Tusker ikiwa ni kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC utakaochezwa Oktoba 30, kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic