October 14, 2013




Mshambuliaji nyota wa Yanga, Mrisho Ngassa amesema atachoma moto nyumba zake tano iwapo hataifunga Simba Jumapili.


Ngassa amesema hasira zake ni kama atashindwa kufunga au angalau kutoa pasi itakayozaa bao litakaloimaliza Simba.

“Niko vizuri na ninajiona niko tayari kwa mchezaji, nataka kufanya kazi nzuri na ninajua Simba nitawafunga.

“Kama nitashindwa kufunga basi nitatoa angalau pasi ya bao litakalosababisha Simba wafungwe. La sivyo nitachoma nyumba zangu tano ninazomiliki,” alisema Ngassa akionyesha kujiamini.

Ngassa ametua Yanga baada ya kuichezea Simba kwa mkopo aliyojiunga nayo akitokea Azam FC.

Lakini alilazimika kulipa faini ya Sh milioni 15 baada ya kubainika alisaini mkataba na kuchukua Sh milioni 30 za Simba.

Yanga na Simba zinakutana Jumapili katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Simba ndiyo wanaoongoza ligi hiyo kwa kuwa na pointi 15 lakini inaonekana bado ni vigumu kumtabiri atakayeibuka na ushindi siku hiyo.
Ligi hiyo imekuwa ngumu na ya ushindani sana na timu zimekuwa zikichuana vikali katika kila mechi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic