October 14, 2013

CHANONGO AKIWA KAZINI SIMBA DHIDI YA TIMU YA VIJANA YA OMAN

Beki kiraka wa Yanga, Mbuyu Twite amemwambia winga wa Simba, Haroun Chanongo kuwa ajiandae na ushindani katika mechi yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara.


Timu hizo pinzani zinatarajiwa kuvaana Oktoba 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, mechi inayotarajiwa kuwa ushindani mkubwa.

 Twite amesema  amejiandaa vya kutosha kuhakikisha anakabiliana na mchezaji wa timu pinzani atakayekabana naye ambaye ni Chanongo.
Twite alisema, katika mechi hawataki kupoteza na badala yake washinde ili wawashushe wapinzani kwenye msimamo wa ligi kuu.

“Ujue kwenye mechi yetu na Simba tunahitaji ushindi wa aina yoyote ili tuwashushe kwenye msimamo wa ligi kuu na sisi tupande tuongoze.

“Hivyo mchezaji atakayepangwa kucheza upande wangu namba saba (Chanongo) basi ajiandae vyema, sitaruhusu krosi yoyote ipigwe kwenye goli letu,” alisema Twite.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic