October 14, 2013

KAZIMOTO KAZINI...



Kiungo wa zamani wa Simba, Mwinyi Kazimoto alirejea nyumbani jijini Dar es Sakaam kimyakimya.


Hata hivyo, Kazimoto anayekipiga katika timu ya Al Markhiya alirejea nchini Qatar kimyakimya na kuendelea kuichezea timu yake.

Rafiki wa Kazimoto alithibitisha kuhusiana na ujio wa kimyakimya wa Kazimoto.

“Kweli alikuwa hapa Dar, lakini amekaa siku mbili tu na kuondoka zake, karudi Qatar,” alisema rafiki huyo.

SALEHJEMBE ilimsaka Kazimoto akiwa nchini Qatar ambaye alithibitisha hilo: “Kweli, sasa niko tena Qatar, kulikuwa na kazi lazima niimalize kabla ya kurudi.

“Sasa nimerejea na ninaendelea na kazi kwa kuwa Oktoma 19 ligi inaanza tena maana ilisimama kutokana na mechi za timu ya taifa ya hapa,” alisema Kazimoto ambaye tayari amejihakikisha namba katika kikosi cha Al Markhiya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic