January 31, 2014


Azam imeweka rekodi kuwa klabu ya kwanza nchini ambao uwanja wake utatumika katika michuano iliyo chini ya Shirikisho la Soka la Kimataifa, Afrika.


Azam FC imeweka rekodi hiyo baada ya Caf kuupitisha uwanja wake kutumika katika michuano ya Kombe la Shirikisho.

Azam itaanza kazi na Ferreviario ya Msumbuji na ililazimika kufanya ukarabati wa nguvu ili kufikia viwango vinavyotakiwa
Mkurugenzi wa mashindano wa Caf, Khaled Naser amethibitisha kuhusiana na hilo na sasa unakuwa uwanja wa kwanza wa klabu kutumika chini ya Caf.
Kabla ya hapo, klabu zote zikiwemo Simba, Yanga, Mtibwa Sugar, Pamba ya Mwanza na nyingine zilizowahi kushiriki michuano ya Caf zimekuwa zikitumia viwanja vya CCM au vile vya serikali.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic