Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji bora wa soka
duniani.
Ronaldo ametwaa
tuzo ya Ballon D’or dakika chache zilizopita na kumpiku Lionel Messi ambaye ni
mpinzani wake mkubwa.
Mara baada ya kukabidhiwa, huku akionyesha kweli Ronaldo alipania kuibeba tuzo hiyo safari hii, alijikuta akimwaga chozi mbele ya gwiji la soka duniani, Pele.
Ronaldo mara ya mwisho aliibeba tuzo hiyo mwaka 2008 wakati akiitumikia Manchester United aliyoiwezesha kubeba ubingwa wa Ulaya na Dunia, kabla ya baadaye kuhamia Real Madrid.
Tokea tuzo hizo zilipoanza kuendeshwa na Fifa, hakuna mchezaji aliyewahi kushinda zaidi ya Messi ambaye alizitwaa mara tatu mfululizo.

Lakini leo
kwa mara ya kwanza, Ronaldo kama alivyokuwa akipewa nafasi hiyo kweli ameshinda
na kumbwaga Messi.
0 COMMENTS:
Post a Comment