July 24, 2014



Uongozi wa Yanga umesema unaendelea kusubiri barua ya kutoka TFF inayowaeleza kuhusiana na ushiriki wao.
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu amezungumza na SALEHJEMBE jioni hizi na kusema
Yanga bado itashiriki michuano hiyo.

“Watu wamekuwa wakitaka kujua kama tunashiriki au la, sisi bado ni washiriki.

“Hatujakaa kujadili suala la kujitoa au vingine, hivyo bado tunasubiri TFF watuletee barua, unajua suala la utaratibu ni zuri.

“Hatujui kama kuna utaratibu umebadilika, au uleule. Hivyo tunaamini barua itakuwa ni maelekezo mazuri.

“Kama ikifika mapema itakuwa vizuri pia kwa kuwa ndege tunayoitegemea zaidi ni Rwanda Air, hivyo tukipata barua mapema ambayo inatueleza viongozi wangapi, wachezaji wangapi, basi litakuwa jambo jema,” alisema Njovu na kuongeza.

“Nilisikia TFF wangeleta barua leo, lakini hadi naondoka ofisini jioni hii sikuona. Basi kama wamebanwa, wangeweza hata kututumia barua pepe ili tuwe na uhakika.

“Yanga na TFF ni taasisi kubwa, hivyo ni vizuri kufanya mambo kwa kufuata utaratibu na barua ni jambo zuri zaidi.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic