September 14, 2020


 KOCHA wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amefichua kuwa kwa jinsi kikosi cha Yanga kilivyo msimu huu itachukua muda kuwafikia wapinzani wao Simba.

 

Julio amesema: “Ukiangalia Simba tayari wameshakaa muda mrefu wakiwa pamoja na hata ukiangalia walivyocheza kwenye Ngao ya Jamii tayari walikuwa wakicheza kitimu tofauti na Yanga ambao bado wanajenga timu yao kutokana na wachezaji wengi kuwa wapya.


“Ukweli itawachukua muda kukaa sawa ili kuweza kwenda na kasi ya ligi lakini Yanga pia kocha anatakiwa kuwa makini katika ubadilishaji na upangaji wa kikosi.


"Mchezaji kama Kaseke,(Deus) anatakiwa kucheza ila sio muda mrefu na kiungo mpya yule Farid Mussa anaonyesha ana kitu hivyo ni suala la kusubiri na kuona nini kitatokea kwao ila wanapaswa kuwa na subira."


Yanga jana ilishinda kwa ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mbeya City na kuvunja rekodi ya msimu uliopita kwa kushindwa kuvuna pointi tatu kwenye mechi zote mbili.


Bao pekee la Yanga lilipachikwa kimiani na beki kisiki, Lamine Moro kwa kichwa ndani ya 18 akimalizia kazi ya kona iliyochongwa na Muangola, Carlos Carlinhos ambaye aliingia uwanjani dakika ya 60 akichukua nafasi ya Feisal Salum.


20 COMMENTS:

  1. Si kwa maandamano yale ya kuwapokea akina mukoko yanga wamepigwa. Ni wachezaji kawaida sana huwezi kuwafananisha kiuwezo na akina Muzamiru,khasani Dilunga na kabunda wa kmc. Hawa wazawa wapi vizuri zaidi yao tena sana.Mechi ya mbeya city kama yanga atacheza vile kwenye mechi ya simba basi yanga watamfukuza kocha yaani yanga wanatabika kupata matokeo mazuri nyumbani na timu zenye wachezaji wa kawaida licha ya kelele zote zile za usajili.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeambiwa tofauti ni kuwa Yanga ni timu mpya na Simba wako pamoja muda mrefu sasa bado unaendelea kufananisha Yanga na Simba hivi watu mlisoma wapi unashindwa kuelewa sentensi fupi tu? Yanga ikikaa pamoja kama timu itakuwa timu nzuri sana kwasasa hivi wanaijenga timu!

      Delete
    2. Kwani wachezaji wa Mtibwa walioisumbua Somba juzi au wa Ihefu (hadi wana dhurumiwa goli) sio wachezaji wazawa unaowaita wa kawaida tu?! Chama, Morrison na Bocco walifichwa kabisaa, Kapombe akashindwa kupanda; dimba lote la kati likimilikiwa na Mtibwa?
      Eleweni kitu kimoja, kwamba mwaka huu ligi ni ngumu; timu zimepungua na zinashuka 6, kila mmoja yuko makini.
      Haji Manara alisema Simba watashinda mechi zote 28 za awali tena bila kufungwa goli. Ebu nambie yako wapi, Manula katunguliwa tena bila utetezi.
      Zile tamho kwamba Simba itatumia timu 2 kwa mechi tofauti ili kupunguza uchovu, thubutu; ebu jaribuni na bado mnaweza shangazwa na Biashara United.

      Delete
  2. Hujaelewa alichosema Julio, nakusaidia; amesema wapewe muda sasa wewe unafanya judgement kwa game mbili tu. Ubora wa wachezaj wa Yanga utaujua tutakapocheza na Simba tu. Mbona hata walivokuja Sevilla kucheza na Simba wachezaj wa Simba mliwaona wazuri kuliko wa Sevilla lkn je ilikuwa kwel kwamba Simba Ni wazr kuliko Sevilla

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe kweli bange, wenzako tunawaza ubingwa ww unawaza kumfunga Simba, hata hivyo mkiendelea kuunganidha team Simba atakuwa amekaka anawatazama tu? Hamna visingizio hapo utopolo. Chaka kingine hlo

      Delete
  3. Bora Ni Bora tu, utopolo pale mmeingia mkenge. Hi
    Mbona onyango ameingia msimu huu tu lkn Ni noma balaa. Kagere alivyoingia tu akawa Ni noma mpaka leo, Tambwe alivyoingia tu akawa Ninoma. Pale mmeingia chaka, wenzenu wanajiandaa na ligi ninyi mlikuwa mnabebana na kujiandaa na utpopolo day. Ndo mjifunze mpira wa miguu cyo rede

    ReplyDelete
  4. Maandalizi yenu yamwkuwa duni toka mwanzo.

    ReplyDelete
  5. Ni kweli wachezaji wako vizuri wapewe muda Ili kupata muunganiko(Chemistry), pia ikumbukwe ikumbukwe kila team inapambana kupata points 3.

    ReplyDelete
  6. Hv c mkamuombe RAGE akawafutie hili jina RITA!

    ReplyDelete
  7. Hv c mkamuombe RAGE akawafutie hili jina RITA!

    ReplyDelete
  8. Utopolo mnaakili za kibabubabu mnawaza kumfunga Simba tu, Simba tunawaza kuchukua ubingwa na tushaanza hivyo moja lishaingia ndani tayari.

    ReplyDelete
  9. Povu linawatoka nguruwe fc la nini? Mikia mmeshinda game ngapi na muna pointi ngapi hamjiulizi tu? Timu mulizocheza nazo si za kawaida tu!?Ihefu, mtibwa hamjapata shida kupata matokeo? Na mjue mpira hauna ugenini wala nyumbani popote unashinda tu.kwa kiwango anachoonesha simba siyo ya kuitabilia makubwa ni litimu la kawaida sana, kiwango kibovu licha ya kukaa pamoja kwa muda mrefu,bado kiwango kibovu sana.

    ReplyDelete
  10. We hapo juu unaongea pumba simba kacheza ugenini na wachezaji wake wazawa lakini matokeo kama ulivyosikia. Ihefu kwenye mechi yake ya raundi ya pili kampiga mkwasa na ruvu shooting yake na uzoefu wake wa ligi kuu. Ifananishe simba ya mkapa kwenye mechi zijazo na yanga ya mkapa iliosumbuka kwa kibonde mbeya city.

    ReplyDelete
    Replies
    1. True! utopolo wamebebwa na tff waanzie nyumbani Kama caf wanavyopanga kwa tem zenye uwezo mdogo ili zijiamini lkn bdo mnambwela.

      Delete
    2. Week bdo hujui soka kaa kimyaaaa Kama huelew

      Delete
    3. ๐Ÿ˜†๐Ÿ˜† unajidifu kumfunga mbeya city kwa mkapa. Ila sishangai maana Ni mbabe wako na pia ndo uwezo wenu hongera utopolo.

      Delete
  11. sometimes ukikutana na baadhi ya mashabiki mitandaoni inabidi ukae kimya tu ili msionekane wote wajinga.kuna aina ya mashabiki mimi hupenda kuwaita mashabiki maandazi,wao siku zote wanawaza kubishana tu hata katika mambo ambayo yako wazi na hayahitaji kubishana.ukiwafuatilia sana mashabiki wa dizaini hii utagundua hakuna la msingi wanalolijua kwenye soka zaidi ya kuanzisha ubishi wa kipumbavu,wakati mwingine hata ukimwambia akutajie first eleven ya timu yake haijui.na kikubwa zaidi wengi wao ukiwafiuatilia utakuta hata shule hawajaenda....KAMA HAO MASHABIKI WA SIMBA HAPO JUU.

    ReplyDelete
  12. Lawama zangu zote naziamishia kwa kocha wa mbeya city hakuelewa ili kupata sare kocha mwenyewe unahitaji kujua team wap imeelemewa na sio kuacha wazuie na kusababisha Kona na faulo zisizo kuwa na faida huku hakusoma akili ya benchi la ufundi la yanga kukuingiza carhinos

    ReplyDelete
  13. Washukulu TFF kuwapa mechi 2 kuanzia uwanja taifa wangeanza kma simba alivyoanzia ugenini sasa hv tungesema mengne

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kobelo za kulamuka?
      Hivi kweli Simba ana ugeni gani Morogoro?
      Miaka yote 2 iliyopita kajishindia goli 3-0, juzi ndo ahenyeke vile au Mo hakutoa neno?
      Uwanja wa Sokoine meaka jana Simba kashinda mechi zote dhidi ya Mbeya City na Prison, ndo mwaka huu asotee pointi kwa Ihefu hadi wakanyimwa goli halali kabisa?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic