December 2, 2014


Kiungo wa Chelsea, Nemanja Matic amesema pamoja na kucheza mechi 20 bila kupoteza, lakini anawaonya wenzake.
Amesema kucheza mechi hizo bila ya kupoteza, si sababu kwamba wana uhakika wa kutwaa ubingwa.
Kwa LIgi Kuu England, wameishacheza mechi 11 bila ya kupoteza.
Matic amesema wakati akiwa Benfica walicheza mechi 28 bila ya kupoteza, lakini mwisho wakakosa ubingwa.
“Umakini ndiyo jambo muhimu na tunalazimika kuwa makini sana,” alisema Matic.
Matic ndiyo jembe kwenye kiungo cha ukabaji cha Chelsea kwa sasa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic