Kikosi cha Simba imeendeleza kufanya ubabe katika mechi zake za
kirafiki visiwani hapa, baada ya juzi kushinda mchezo wake wa tatu mfululizo
ilipoizabua timu ya Polisi inayoshiriki Ligi Kuu Zanzibar kwa mabao 2-0 kwenye
Uwanja wa Amaan.
Matokeo hayo yamempagawisha kocha msaidizi wa timu hiyo, Suleiman
Matola ambaye amesema kiwango cha wachezaji wake kimepanda na wanachosubiri ni
kufanya maangalizi tu kwenye ligi kuu.
Awali, Simba iliichapa Kombaini ya Zanzibar na baadaye ikainyuka Black
Sailors.
Katika mchezo wa juzi, mkongwe Mussa Hassan Mgosi aliwainua
mashabiki a Simba dakika ya pili kwa bao safi akiunganisha krosi ya kushoto ya
beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’. Mshambuliaji mwenye nguvu aliyetamba atavaa
viatu vya Okwi, Elius Maguli alipiga bao jingine baada ya kuitendea haki kazi
nzuri iliyofanywa na beki Kessy Ramadhan.
“Ujio wa Mwinyi Kazimoto nao umetuletea hamasa kubwa, kwa hiyo
kikosi kipo vizuri na tunatarajia kufanya mambo makubwa ligi itakapoanza,”
alisema Matola baada ya mchezo huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment