GOOOOOOOOOOOOO Dk 90+5 Kamusoko anafunga bao kwa mfumo wa baiskeli baada ya pasi ya kichwa ya Ngoma baada ya krosi safi ya Mwinyi.
Mwinyi anapiga krosi safi, nusura mpira uingie ndani ya lango la Sports
Dakika za mwisho, Sports wanaonekana kuridhika na sare, wanapoteza muda kwa kujiangusha mara kadhaa, hata hivyo Yanga wanaonekana kutokuwa na kasi yoyote inaweza kusaidia kubadili matokeo tofauti na sare
+5Dk 88, Kamusoko, Bossou na Dida wanambeba mchezaji wa Sports aliyekuwa ameumia na kumpeleka nje
Dk 86, Busungu anafanya jaribio lake la kwanza kwa kugeuka na kupiga shuti kali. Lakini kipa Sports anadaka kwa ustadi kabisa
SUB Dk 83 Yanga wanamtoa Kaseke na nafasi yake inachukuliwa na Mwashiuya
Dk 80, Sports wanapoteza nafasi nzuri kabisa baada ya Juma Abdul kujichanganya na Ally Ramadhani anashindwa kuifungia Sports kwa kupiga mpira unaotoka nje
Dk 79, krosi nyingine nzuri ya Mwinyi tena lakini Sports wanaokoa
SUB Dk 75 Yanga inamtoa Amissi Tambwe anaingia Malimi Busungu
Dk 74, Msuva anapiga shuti kali lakini kipa Sports anadaka kwa ufundi
Dk 66 hadi 70, bado inaonekana timu zinashindwa kuweka mpira chini sana kutokana na ubovu wa uwanja. Hofu ya kupoteza mpira inawatawala wachezaji. Hadi sasa hakuna shambulizi kali
Dk 65, Dida naye anachupa kudaka mpira wa tik taka wa Pera ambao ulikuwa hatari katika lango la Yanga
Dk 62, Yondani analazimika kufanya kazi ya ziada kuokoa
Dk 56 hadi 60, bado mpira unachezwa katikati na umepooza sana. Hakuna mashambulizi ya nguvu na kila timu inaonekana haina mipango bora ya kufika katika lango la timu pinzani
Dk 55, Kaseke anapata mpira akiwa anamtazama kipa, lakini Meddy wa Sports anajitoa na kuokoa. anamgonga Kaseke sasa yuko chini
Dk 50, Mwinyi anapiga krosi nzuri ya mpira wa adhabu, Bossou anapiga kichwa juuuuu
Dk 50 Ally Ramadhani anaingia kuchukua nafasi ya Fadhili Kizenga kwa African Sports
Dk 46, Yanga ndiyo wanakuwa wa kwanza kufanya shambulizi, krosi safi ya Msuva lakini Sports wanakuwa imara kuondosha
MAPUMZIKO Dk 45+3 Yanga wanapiga kona, Juma Abdul anapiga ti tak lakini African Sports wanaokoa tena
Dk 44, Ngoma anaruka juu kuuwahi mpira anapiga kichwa lakini dhaibu
Dk 39 hadi 42, mpira unachezwa zaidi katikati ya uwanja na hakuna mashambulizi makali kwa upande wowote ule
SUB Dk 37 Meddy James anakwenda nje kwa African Sports anaingia Mohammed Issa
Dk 33 Kaseke anapiga krosi safi inatua kichwani kwa Kamusoko, lakini kipa anaudaka kwa ufundi kabisa
KADI Dk 31, Pera Mohammed wa African Sports analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Kamusoko
Dk 30, Ngoma anajaribu kupiga shuti kali, lakini linapaa juu ya lango. Bado hakuna mashambulizi makali kwa pande zote
Dk 24 Yanga wanapata kona, inachongwa na Juma Abdul, lakini haina madharaDk 21, Msuva anaingia ndani ya sita ya African Sports lakini anapiga shuti kuuuubwaaaa
Dk 7 hadi 12, mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja, hakuna mashambulizi makubwa na uwanja kuwa na kiwango duni unaonekana kuwa moja ya pingamizi
Dk 6 African Sports wanapata kona baada ya Yondani kuutoa mpira nje. Lakini inakuwa ni kona isiyo na madhara
Dk 5 Msuva anapiga tik tak, lakini kipa anaruka na kudaka vizuri sana
Dk 4 Yanga wanapata mkwaju wa adhabu, Haji Mwinyi anaichonga, unamgonga Msuva na kutoka nje.
Mechi imeanza na Yanga ndiyo wanakuwa wa kwanza kufika katika lango African Sports, lakini linakuwa si shambulizi la kali.
Mechi imeanza na Yanga ndiyo wanakuwa wa kwanza kufika katika lango African Sports, lakini linakuwa si shambulizi la kali.
0 COMMENTS:
Post a Comment