April 14, 2016


Mashabiki wa Al Ahly wameondoka na nembo ya klabu ya Simba kwenda nayo Cairo kwa ajili ya kuonyesha shukurani yao kwa Simba.

Mashabiki hao waliokuwa wanaishi eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam, wanajiandaa kutengeneza bendera kubwa ya Simba ambayo wataitumia wakati wakishangilia timu yao itakapokuwa inapambana na Yanga katika mechi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mechi ya kwanza, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 jijini Dar es Salaam. Mashabiki wa Simba walikuwa wakiwasaidia kushangilia wakiungana na mashabiki wao wa Ultras.


“Tukiwafunga tu, tutaitumia bendera ya Simba kuionyesha wakati tunashangilia. Tunafanya hivyo kuonyesha shukurani yetu kwao,” alisema mmoja wa mashabiki hao ambao kundi la mwisho liliondoka jana kurejea Cairo kuisubiri Yanga wiki ijayo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic