Kikosi cha Azam FC kikiwa chini ya Kocha Mhispania, Zeben Hernandez kimeanza vizuri mechi zake za kujipima kwa ajili ya maandalizi ya kikosi kipya kwa kuichapa Ashanti United kwa mabao 2-0.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, leo, Azam ilifunga mabao yake yote mawili katika kipindi cha pili.
Kiungo dogo, Mudathir Yahya ndiye alikuwa wa kwanza kufunga bao katika dakika ya 69 na baadaye Masoud Abdallah akapachika la pili.
Kiucheza, kiasi wachezaji wa Azam FC walionekana kubadilika na kucheza soka la kujiamini na pasi za uhakika.
Kocha huyo kijana alitaka kuanza kukijaribu kikosi chake ikiwa ni sehemu ya kukitengeneza kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Bara ambayo inatarajia kuanza wiki ya pili ya Agosti.
0 COMMENTS:
Post a Comment