Kampuni itakayoingia mkataba na Yanga chini
ya Mwenyekiti Yusuf Manji, itajenga uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo.
Mmoja wa wajumbe wa baraza la wadhamini,
Francis Kifukwe amethibitisha hilo kwa kusema, kampuni inayokodisha Yanga,
imekubali kujenga uwanja wa mazoezi.
“Kweli kila kitu kinakwenda vizuri na baada
ya muda fulani, klabu itafanya suala la kuingia makubaliano.
“Suala la uwanja ni kweli, tumekubaliana
kuwa lifanyiwe kazi na kampuni hiyo imekubali kujenga uwanja ambao utakuwa
sehemu nyingine. Mbali na pale Jangwani ambako sisi tunataka kujenga uwanja wa
kudumu.
“Tayari kampuni hiyo imetoa mapendekezo
yake, sisi pia tunataka kutoa ya kwetu na kukaa ili kumalizana katika hili,”
alisema Kifukwe.
Manji, aliwaomba wanachama wa Yanga moja ya
kampuni zake kuikodi nembo na timu ya Yanga kwa kipindi cha miaka 10, jambo
ambalo Wanayanga walilipitisha.
0 COMMENTS:
Post a Comment