Kocha wa Simba, Joseph Omog amesema atautumia muda wa kipindi cha siku tatu nne kabla ya kurejea kwenye ligi, kurekebisha tatizo la umaliziaji.
Omog raia wa Cameroon amesema, umaliziaji bado jambo linalowasumbua na muda huo utasaidia.
“Lazima kulimaliza, lakini masuala ya soka ni kujifunza kila siku tena na tena. Hivyo nitautumia muda huu kurekebisha mambo,” alisema Omog.
Simba itacheza na Polisi Dodoma mechi ya kirafiki kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, keshokutwa.
Sehemu ya kipimo kwa mabadiliko ya Omog itakuwa ni katika mechi hiyo kwa kuwa vijana wake wamekuwa wakipoteza nafasi nyingi za wazi za kufunga.
0 COMMENTS:
Post a Comment