February 18, 2013

Beki wa Simba, Shomari Kapombe jana alitibiwa kwa takribani nusu saa baada ya msuli mkubwa wa mguu wake kusimama.
Hali hiyo iliwalazimu zaidi ya madaktari wanne kuanza kumtibu huku muda wote akiangusha kilio kutokana na maumivu makali aliyokuwa anayapata.
Baadaye jopo la waliokuwa wakimtibu waliongezeka hadi Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio', nahodha Juma Kaseja pamoja na msemaji wa klabu hiyo, Ezekiel Kamwaga.
Baada ya matibabu hayo yaliyochukua muda mrefu na kuweka rekodi, Kapombe alibebwa na kuingizwa ndani kuendelea na matibabu.
Daktari wa Simba, Cosmas Kapinga alisema atalizungumzia suala hilo baada ya kumaliza matibabu.
Kapombe aliumia dakika za mwisho katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Libolo ya Angola ambayo ilitawala mchezo na kuilaza Simba kwa bao 1-0.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic