February 18, 2013

Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amesema amefanikiwa kuwaona Azam FC katika mechi yao ya Kombe la Caf dhidi ya Al Nasr ya Sudan Kusini.
Brandts amesema ameona kila alichokuwa anakitaka na anachokifanya ni maandalizi ya mwisho kabla ya mechi yao Jumamosi ijayo.
"Nilitaka kuwaona kwa kuwa ni muhimu katika kipindi hiki bila ya kujali wanacheza mechi ipi na timu ipi.
"Kikubwa ni kuwaona wanacheza, nilichokiona siwezi kusema badala yake kila kitu kitafanyiwa kazi hadi siku ya mechi mambo yataonekana.
"Nasisitiza, nawaheshimu Azam lakini ninachotaka ni ushindi kwa kuwa ndiyo gia yetu kubwa, kama tutashinda, basi ni nafasi ya kwenda kwenye ubingwa," alisema Brandts.
Yanga ina pointi 36 kileleni ikifuatiwa na Azam FC yenye 33 na ndiyo timu zinazoonekana kuchuana huku mabingwa watetezi Simba, wakisuasua katika nafasi ya tatu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic