Baada ya kujiunga na kikosi cha
Etoile du Sahel na kushiriki nacho mazoezi kwa zaidi ya wiki nne bila ya
kucheza mechi, hatimaye kiungo mshambuliaji Emmanuel Okwi amecheza kwa dakika
20.
Okwi raia wa Uganda alicheza mechi
iliyopita ya ligi wakati Etoile ilipokuwa inaivaa Stade Tunisien.
Katibu Mkuu wa Etoile, Adel Githi
ameuambia mtandao huu kuwa Okwi alicheza muda huo na kuonyesha kiwango kizuri.
“Ilikuwa mechi yake ya kwanza
lakini alionyesha ni mchezaji mzuri, tunategemea ataendelea kukua na kufana
vizuri zaidi.
“Sisi hatuna haraka, mambo
yatakwenda hatua kwa hatua na tayari Okwi alielezwa hilo kwamba anatakiwa
kukubaliana na hali.
“Kwa kuwa ameanza kucheza, maana
yake inategemea juhudi zake na mipango ya mwalimu,” alisema.
Aidha, Githi alisema wamempa
ruhusa Okwi ya kurejea Uganda kwa ajili ya kuungana na timu ya taifa ya Uganda
inayojiandaa kuivaa Liberia ugenini mjini Monrovia.
Okwi alijiunga na timu hiyo
akitokea Simba kwa dau la dola 300,000, fedha ambazo Simba wamekuwa wakisotea
kuzipata.
0 COMMENTS:
Post a Comment