Beki wa Chelsea, John Terry ametoa
kali ya wiki baada ya kuamua kulitelekeza gari lake lenye thamani ya pauni 175,000
(Sh milioni 437) barabarani na kurejea zake nyumbani.
Nahodha huyo wa Chelsea alichukua aumuzi
wa kuliacha gari hilo aina ya Bentley kutokana na foleni kubwa iliyomchosha na
kuamua kuliacha.
Lakini kwa wanaoishi Dar es Salaam,
kama Terry angeishi angalau mwezi mmoja katika jiji hili maarufu kwa foleni, basi
inawezekana kila siku angejikuta akitembea kwa miguu kurejea nyumbani huku
agari akiliacha barabarani.
Akiwa katika barabara ya A3, magari
hayakuwa yakisogea mbele, hali iliyomfanya aombe msaada kwa mtu anayemfahamu
ili aifanye kazi ya kulipeleka kwake iwapo foleni itapungua.
Kabla ya Terry maarufu kama JT
kuamua kuliacha gari hilo, watu wengine pia walionyesha kuchoshwa na foleni
hiyo na kuteremka kwenye magari yao na kuanza kupiga stori.
Terry aliona hana sababu ya kupoteza
muda, hivyo akateremka na kuachana na gari hilo lenye thamani kubwa.
Foleni hiyo kubwa ilisababishwa na
mtu mmoja aliyeamua kujirusha darajani ili apoteze maisha. Wakati huo waokoaji
walikuwa wamefika katika eneo la tukio kwa ajili ya uoakoaji.
Juhudi zao za kuokoa roho ya mtu
huyo ilishindikana baada ya kufia katika gari la wagonjwa wakati madaktari
wakijaribu kuokoa uhai wake.
0 COMMENTS:
Post a Comment