Kama ulikuwa unafuatilia soka ya Tanzania, hakika utakuwa
haujamsahau mshambuliaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi.
Huyu jamaa ni raia wa Uganda, inawezekana kabisa ndiye
alikuwa mchezaji hatari zaidi kuliko wengine wote walioshiriki misimu miwili
iliyopita ya Ligi Kuu Bara.
Tokea ameondoka Simba na kujiunga na Etoile du Sahel
takribani miezi minne iliyopita, tayari kumekuwa na tatizo kubwa ndani ya klabu
hiyo hiyo.
Achana na tatizo la uongozi kulumbana, mfano mkutano wa leo
asubuhi Jumapili ambao unanuia kuung’oa uongozi, lakini kikosi cha Simba
kimeyumba kabisa!
Uchezaji umebadilika na hata mashambulizi ya Simba yamekuwa
si yale yaliyokuwa yakifanyika katika mechi za msimu uliopita.
Hapa cha kujiuliza tatizo ni uwezo wa Okwi umeathiri Simba,
au kuondoka kwa aliyekuwa Kocha Mkuu, Milovan Cirkovic. Au mgogoro kati ya
viongozi?
Maswali yanaweza kukosa majibu au majibu yakawa ya
kujikanganya, lakini siku ya mwisho, Okwi alikuwa mhimili mkubwa wa
mashambilizi ya Simba.
Sasa hapo ndiyo pa kuweka swali la msingi, Simba itaendelea
kuyumba kwa muda gani bila ya kuwa na Okwi?
Tanzania nzima, hakuna mshambuliaji mwenye uwezo au kipaji
kama cha Okwi?
Je, nini cha kufanya baada ya hapo ili kikosi cha Simba
kikawe sawa. Hapa kuna mambo mengi sana ya kujifunza kwa Simba ukianzia uongozi
wa juu, wachezaji na hata mashabiki we klabu hiyo.
KAZI KWENU.
0 COMMENTS:
Post a Comment