Mechi ya Ligi Kuu
ya Vodacom kati ya Ruvu Shooting na Yanga iliyochezwa jana Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam imeingiza sh. 62,228,000 kutokana na watazamaji 10,929.
Viingilio katika
mechi hiyo namba 146 iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0
vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata
mgawo wa sh. 14,336,764.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa
ni sh. 9,492,406.78.
Mgawo mwingine wa
mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,289,880.48, tiketi sh. 4,136,390,
gharama za mechi Sh. 4,373,928.29, Kamati ya Ligi sh. 4,373,928.29.
Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,186,964.14, Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 850,486.06 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar
es Salaam (DRFA) sh. 850,486.06.
0 COMMENTS:
Post a Comment