Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeteua waamuzi kutoka Angola kuchezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Morocco (Lions of the Atlas).
Mechi hiyo ya kundi
C itachezwa Machi 24 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Ivory
Coast ndiyo inayoongoza kundi hilo ikiwa na pointi nne na kufuatiwa na Taifa
Stars yenye pointi tatu.
Mwamuzi wa mechi
hiyo ni Helder Martins de Carvalho wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Inacio
Manuel Candido huku Ricardo Daniel Cachicumi akiwa mwamuzi msaidizi namba
mbili. Mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Antonio Muachihuissa Caxala.
Waamuzi hao
watawasili nchini saa 1.20 usiku Machi 22 mwaka huu kwa ndege ya Kenya Airways
wakitokea Luanda, Angola kupitia Nairobi, Kenya.
Kamishna wa mechi
hiyo atakuwa David Fani kutoka Botswana anatarajiwa kuwasili Machi 22 mwaka huu
saa 1.45 usiku kwa ndege ya South African Airways.
Naye mtathmini wa
waamuzi (referee assessor) Neermal Boodhoo kutoka Afrika Kusini atawasili
nchini Machi 22 mwaka huu 1.45 usiku kwa ndege ya South African Airways.
TAIFA STARS YAINGIA
KAMBINI KUIWINDA MOROCCO
Taifa Stars imeanza
kambi jana jioni (Machi 16 mwaka huu) ambapo wachezaji 14 kati ya 23 walioitwa
wameripoti na kufanya mazoezi leo asubuhi chini ya Kocha Kim Poulsen.
Wachezaji
walioripoti ni nahodha Juma Kaseja kutoka Simba na msaidizi wake Aggrey Morris
wa Azam, Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga),
Nassoro Masoud Cholo (Simba), Shomari Kapombe (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
Wengine ni Athuman
Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto
(Simba), Mrisho Ngasa (Simba) na Simon Msuva (Yanga).
Wachezaji Hussein
Shariff, Issa Rashid na Shabani Nditi ambao timu yao ya Mtibwa Sugar jana
ilicheza mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) mjini Turiani wataripoti kambini
leo jioni.
Kikosi hicho
kitakamilika Jumanne asubuhi baada ya wachezaji walio katika kikosi cha Azam
nchini Liberia kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho kurejea nchini. Mbwana
Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemorasi ya
Congo (DRC) wanatarajiwa kutua nchini kesho usiku.
0 COMMENTS:
Post a Comment