Katika
mechi za awali kuwania kucheza Kombe la Dunia, timu ya soka ya Tanzania, Taifa
Stars ndiyo iliyong’ara zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Stars
ndiyo imeibuka na ushindi mnono zaidi kwa kuichapa Morocco ambacho ni kigogo
cha Afrika kwa mabao 3-1 jana kwenye Uwanja wa taifa, Dar es Salaam.
Timu
nyingine iliyofanya vizuri katika ukanda huo ni Ethiopia iliyokuwa nyumbani
Addis Ababa na kuishinda Botswana kwa bao 1-0.
Baada
ya Stars na Ethiopia, timu nyingine za Afrika Mashariki na Kati ziliambulia
vipigo na sare tu.
Kenya
ikiwa ugenini, ilikomaa na kutoka sare na Nigeria huku wenyeji wakisawazisha
bao katika dakika za nyongeza. Harambee Stars iko chini ya kocha wake mpya,
Adel Amrouche, Mbeligiji mwenye asili ya Algeria ambaye kabla alikuwa akiinoa
Burundi.
Rwanda
ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Amahoro, Kigali imekutana na kipigo cha mabao 1-2
kutoka kwa Mali, Liberia ikaifunga Uganda 2-0, Ghana ikaifumua Sudan kwa mabao
4-0 uku DR Congo wakienda sare ‘tasa’ dhidi ya Libya.
Pamoja na ushindi, Stars ilionyesha soka la kuvutia na kuwafanya Wamorocco pamoja na uzoefu wao wa michuano ya kimataifa, wajikute wakitafuta mpira kwa 'tochi' mchana kweupee.
0 COMMENTS:
Post a Comment