Kocha
Mkuu wa Morocco, Rachid Taoussi amekiri kuwa yuko katika wakati mgumu kutokana
na matokeo ya mechi ya jana.
Taoussi,
mmoja wa makocha wenye heshima kubwa nchini Morocco amesema ana kibarua kikubwa
cha kufafanua kuhusiana na kipigo hicho.
“Soka
ni kitu cha ajabu sana, unaweza kufanya mambo mengi sana kuhusiana na soka,
lakini yote yakasahaulika ndani ya dakika tisini.
“Ni
kawaida kama utasikia kesho sina kazi tena kwa kuwa leo tumepoteza, tena
matokeo ambayo yataumiza kila moyo wa mtu wa Morocco mpenda mpira.
“Sisi
tuliokuja na timu hapa Tanzania tumeumia zaidi, lakini wale ambao hawajaona
wanaweza kuumia zaidi kwa kuwa hawajui kiasi gani tulipambana,” alisema.
Lakini
mmoja wa waandishi aliyekuja nchini na timu hiyo ya taifa ya Morocco alisema
huenda kocha huyo anaweza kupoteza kazi yake kwa kuwa kipigo alichopata kutoka
kwa Tanzania ni kikubwa sana na Wamorocco hawataelewa.
Taoussi
amekuwa kocha wa timu za vijana za Morocco, kocha msaidizi wa timu hiyo lakini
amewahi kuzifundisha timu kubwa za Morocco kama FUS Rabat, Waydad Casablanca na
MAS Fez na kufanikiwa kutwaa Kombe la Shirikisho na Super Cup Afrika.
Jana
timu yake ilikutana na kipigo kikali kutoka kwa Stars kwa kuchapwa kwa mabao
3-1 katika mechi ya kuwania kucheza Kombe la Dunia.
0 COMMENTS:
Post a Comment