March 10, 2013




Pamoja na kuandamwa na vituko, mshambuliaji Carlos Tevez ameivusha Man City hadi nusu fainali ya Kombe la FA.

Tevez ambaye huenda akafungwa jela miezi sita kutokana na kukamatwa akiendesha gari baada ya kuwa amezuiwa kufanya hivyo na Polisi leo ameibuka shujaa kwa kufunga mabao matatu katika ushindi wa Man City wa mabao 5-0 dhidi ya Barnsley.

Muargentina huyo alipiha hat trick na kuifanya Man City iwe na uhakika na Silva na Kolarov wakaongeza mbili.


Wengi waliamini Tevez asingeweza kucheza kutokana na tatizo hilo linalomkabili la kukutwa akiendesha gari wakati tayari alikuwa na adhabu.

Katika mechi hiyo, City waliwapeleka puta wapinzani wao, huku Tevez akionyesha kiwango cha juu kwa kuwasuambua sana mabeki wa Barnsley.

Juzi alitakiwa kurudi polisi keshokutwa ili suala lake lianze kushughulikiwa na mara moja ijulikane kama atafikishwa mahakamani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic