ALEXANDRE Lacazzette anatazamiwa kuanza mazoezi wiki hii baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.
Mshambuliaji huyo raia wa Ufaransa hajaichezea Arsenal karibu mechi saba kutokana na kuumia kwenye mechi dhidi ya Tottenham Hotspur.
Kupona kwake ni habari njema kwa timu yake ataongeza ukali wa Safu ya ushambuliaji iliyokuwa chini ya Pierre Aubameyang.
Katika mechi tatu alizocheza msimu huu kabla hajaumia alitupia jumla ya mabao mawili.
0 COMMENTS:
Post a Comment