March 17, 2013




Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Azam FC wanatarajia kuingia uwanjani kupambana na Barrack ya Liberia mjini Monrovia.

Azam wanashiriki Kombe la Shirikisho ikiwa ni baada ya kuing’oa Al Nasiri ya Sudan Kusini na ndiyo timu pekee ya Tanzania inayoshiriki michuano ya kimataifa baada ya Simba kutolewa na Libolo ya Angola.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Idd Maganga amesema dakika chache zilizopita kwamba kikosi chao kiko katika hali nzuri na wasubiri pambano hilo.

“Tunaendelea vizuri kwa kweli, kila kitu kiko vizuri na tunashukuru leo hali ya hewa ni nzuri. Jana kulikuwa na mvua lakini leo mambo ni safi sana. Hivyo tuko tayari kwa mapambano,” alisema Maganga.

“Kuhusiana na muda, hapa tutaingia uwanjani saa 10 kamili ambayo nyumbani (Tanzania) itakuwa saa moja.”

Salehjembe inawaombea Azam  FC kila la kheri katika mechi hiyo kwa kuwa matokeo mazuri Monrovia, ni njia nzuri ya kusonga mbele Dar es Salaam.

KILA LA KHERI VIJANA.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic