April 6, 2013



Bayern Munich wametawazwa kuwa mabingwa wa Bundesliga ikiwa ni baada ya kupata pointi tatu nyingine kwa kuichapa Eintracht Frankfurt  bao 1-0  kwenye uwanja wa nyumbani mjini Frankfurt.

Pamoja na kutwaa ubingwa huo, Munich  imeweka rekodi mpya katika Bundesliga kwa kuwa hakuna timu imewahi kutwaa ubingwa wa ligi hiyo ikiwa imebakiza michezo sita mkononi.

Waliokuwa mabingwa watetezi, Borussia Dortmund nao waliibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya vibonde Augsburg ambao walikuwa wanaongoza kwa mabao mawili kabla ya kuchapwa wao nne.

Schalke nao waliichapa Werder Bremen kwa mabap 2-0, Bayer Leverkusen ikatoka sare ya  1-1 na Wolfsburg, Borussia Moenchengladbach ikaitwanga Greuther Fuerth 1-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic