| Consolata Adam (kulia) na Doris Malulu |
Kinywaji
maarufu cha Grand Malt leo kimezindua tuzo kwa wanafunzi wa elimu ya juu
zijulikanazo kama “Excel with Grand Malt”, huu ukiwa ni mwaka wa tatu kwa tuzo
hizi kutolewa.
Akizungumzia
tuzo hizo, meneja wa kinywaji cha Grand Malt, Consolata Adam alisema, Excel with Grand Malt
ni tuzo za aina yake ambazo zimelenga kutambua na kuthamini mchango wanaoonesha
wanafunzi katika fani mbalimbali nje ya masomo ya darasani.
“Tunatambua
kuwa kazi kubwa ya mwanafunzi anapokuwa chuoni ni kuhudhuria vipindi vya
darasani na kupata elimu, bali tunapenda pia kuwatambua wale wachache ambao
wanakwenda mbali zaidi na kufanya mambo ya maendeleo katika mazingira yao ya
chuo,” alisema.
Tuzo hizi
zilianzishwa mwaka juzi ambapo tuliweza kufika katika mikoa sita na kufikia
vyuo vipatavyo ishirini. Kwa mwaka huu mchakato utaanza mwezi Aprili hadi Juni,
na mikoa itakayohusika ni pamoja na Dar es salaam, Morogoro, Iringa, Dodoma,
Kilimanjaro na Mwanza ambapo vyuo vipatavyo 20 vitashiriki.
Kama ilivyokuwa miaka iliyopita, fani
zitakazoshindanishwa ni Ubunifu (Innovation), Michezo (sports), Utamaduni na
burudani (Culture & Entertainment) na Mazingira na Huduma za jamii
(Environment & social responsibilities). Kama ilivyo ada, washindi katika
fani hizi watajipatia zawadi mbalimbali toka Grand Malt ikiwa ni pamoja na pesa
za kununulia vitabu na vyeti vya ushindi.
Kwa sasa
natangaza rasmi kuwa tunzo hizi zimezinduliwa rasmi na mkoa wa kwanza utakuwa
ni hapa Dar Es Salaa ambapo tunatarajia kufanya tamasha kubwa kwenye viwanja
vya chuo kikuu cha Chuo kikuu Artdhi siku ya jumamosi kisha jumapili tutafanya
tamasha la ufunguzi kwenye Viwanja vya chuo cha Mkwawa mkoani Iringa na
kutakuwa na burudani na zawadi nyingi na zaidi kutakuwa na GrandMalt baridi na
hakutakuwa na kiingilio chochote. Alisema Bi. Consolata.
Akielezea
umuhimu wa Tuzo hizo, meneja masoko wa TBL, Fimbo Butallah alisema: “tunafurahi
sana kuona vyuo vyote vilipokea tuzo hizi kwa furaha kubwa, hii ni kwa sababu
wanatambua umuhimu wake. Kupitia tuzo hizi ambazo zitakuwa zikitolewa kila
mwaka, Grand Malt inatoa changamoto kwa vijana walio vyuoni kuona umuhimu wa
kujituma na kufanya mambo mengi na makubwa zaidi ya kufaulu mitihani ya
darasani tu.
“ Tunaomba
viongozi wa serikali za wanafunzi na viongozi wa vyuo kuendelea kutoa
ushirikiano kama walivyofanya mwaka jana ili kuleta ufanisi zaidi katika tuzo
za mwaka huu. Kama ilivyo kawaida, utaratibu utakuwa ule ule ambapo wanchuo
watapendekeza majina ya vijana wanaoamini kuwa wamefanya mambo makubwa ndani ya
vyuo vyao katika tasnia zilizotajwa hapo awali, kisha kufuatiwa na kipindi cha
kupiga kura ambapo washindi watapatikana.”
Kwa upande
wake Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu alisema GrandMalt kwa kuzingatia
umuhimu wa juhudi za serikali katika kuhamasisha jamii kutunza mazingira kwa
kupanda miti mwaka huu Grand Malt itafanya zoezi maalum kwenye kila chuo kwa
kupanda miti imara itakayosaidia kutunza na kuboresha mazingira ya vyuo hivyo
ili kuandaa mazingira bora ya kusomea ya wanafunzi wa sasa na wa vizazi vijavyo.
Mkoani
Iringa zoezi hilo litafanyika jumatatu April 22,2013 katika vyuo vya
Mkwawa,Ruaha na Tumain na Mkoani Dodoma zoezi hilo litafanyika kwenye vyuo vya
UDOM na St Johns siku ya jumatatu April 29,2013 asubuhi, halafu zoezi
hilo litaendelea katika mikoa ya Morogoro,kilimanjaro,Mwanza na Dar Es Salaam.







0 COMMENTS:
Post a Comment