April 7, 2013



Chelsea imemkaribisha kocha mpya wa Sunderland, Paolo Di Canio kwa kipigo cha mabao 2-1.


Di Canio ndiyo alikuwa ameanza kazi ikiwa ni pamoja na kuandamwa na masuala ya kisiasa kwamba ni shabiki wa siasa za kifashisti. Jana aliendelea kukataa kuzungumzia masuala hayo baada ya mechi.


Mechi nyingine, QPR ilipoteza matumaini ya kubaki Premiership baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi wageni wake Wigan.
Mambo yanaonekana si mazuri na kocha Harry Redknapp amekiri kwamba muziki ni mnene kwao.

Ukiachana na mechi zote, kali zaidi ilikuwa ile ya Tottenham ilipowakaribisha Everton. Matokeo ya mwisho yalikuwa 2-2.

Lakini ngoma ilikuwa si mchezo na timu zote zilicheza mchezo wa kasi ya ajabu, kushambuliana kila upande na mshambuliaji wa Spurs, Emmanuel Adebayor alikuwa kiwembe.


Liverpool nao wakiwa nyumbani Anfield, wakakamatwa na West Ham kwa sare ya bila kufungana. Wenyeji walionekana kupania kuendeleza ushindi lakini mambo yakawa tofauti kabisa baada ya wageni kukomaa.


Nayo Newcastle ikaiathibu Fulham kwa bao 1-0, huku ikifanikiwa kupata ushindi mwishoni. Timu hiyo imekuwa ikipoteza mwelekeo tofauti na msimu uliopita ilionekana ni kiboko cha vigogo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic