April 7, 2013





Ingawa amewaachia pengo la vituko, Mario Balotellio anaonekana hajaacha vituko baada ya kuelezwa atapigwa faini kutokana na kufumwa akivuta sigara kwenye choo cha treni.

Balotelli alikutwa na mhudumu wa treni akivuta sigara wakati wakisafiri kwa ajili ya pambano la Seria A dhidi ya Fiorentina leo Jumapili, pambano hilo lilimalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Hakuna aliyekuwa ameshtukia hali hiyo, hadi mhudumu huyo kwa kwenye treni alipomuambia Naibu Rais wa AC Milan, Adriano Galliani.

Baada ya kuambiwa, mara moja Galliani alimuagiza M’Baye Niang ambaye ni swahiba wa Balotelli akamueleze kuwa ameishabainika na atapigwa faini kwa kitendo hicho.

La Gazzeta dello Sport limesema kitendo hicho kilionyesha kumuudhi Galliani, lakini Balotelli alirejea katika eneo hilo akiwa ni mtu mwenye tabasamu kama hakuna kilichotokea.

Kabla ya kutua AC Milan, Balotelli alikuwa Man City ambako alikuwa akiongoza kwa kuwa mchezaji mwenye vituko zaidi kuliko wote wanaoshiriki Ligi Kuu England.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic