Mechi ya marudiano ya raundi ya
kwanza ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam ya Tanzania na Barrack Young
Controllers II ya Liberia iliyochezwa jana (Aprili 6 mwaka huu) imeingiza sh.
44,229,000.
Fedha hizo katika mechi hiyo
iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa timu hizo kutoka
suluhu zimetokana na watazamaji 17,128 waliokata tiketi.
Viingilio vilikuwa sh. 2,000, sh.
5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000 ambacho kilikuwa kiingilio cha juu kwa jukwaa
la VIP A. Kiingilio cha sh. 2,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo
walikuwa 15,212.
Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo;
gharama za tiketi sh. 5,575,500, asilimia 15 ya uwanja sh. 5,798,025, asilimia
10 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF) sh. 3,865,350 na asilimia 75 iliyokwenda kwa klabu ya Azam
ni sh. 28,990,500.
Mechi iliyopita ya raundi ya awali
ya mashindano hayo kati ya Azam na El Nasir ya Sudan Kusini iliyochezwa kwenye
uwanja huo huo Februari 16 mwaka huu iliingiza sh. 34,046,000 kwa viingilio
hivyo hivyo huku ikishuhudiwa na watazamaji 13,431.
0 COMMENTS:
Post a Comment