Ligi
Kuu ya Bara inaendelea katika raundi yake ya 25 kesho (Mei Mosi) kwa mechi tano
zitakazochezwa katika miji ya Dar es Salaam, Turiani, Morogoro na Mlandizi.
Licha
ya kuwa tayari Yanga imetawazwa kuwa mabingwa wa VPL msimu huu (2012/2013),
mechi dhidi ya Coastal Union itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni
moja kati ya zitakazovuta macho na masikio ya washabiki wa mpira wa miguu
nchini.
Mechi
hiyo namba 172 itachezeshwa na mwamuzi Simon Mberwa kutoka Pwani akisaidiwa na
Said Mnonga na Charles Chambea wote wa Mtwara wakati mwamuzi wa mezani atakiwa
Hashim Abdallah wa Dar es Salaam. Kamishna wa mechi hiyo ni David Lugenge
kutoka Iringa.
Viingilio
katika mechi hiyo itakayoanza saa 10.15 jioni ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya
bluu na kijani, sh. 8,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 kwa VIP C
na B wakati VIP A itakuwa sh. 20,000. Tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mchezo.
Mtibwa
Sugar itakuwa mwenyeji wa African Lyon katika mechi namba 170 itakayochezeshwa
na mwamuzi Dominic Nyamisana wa Dodoma kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Turiani
mkoani Morogoro. Nayo Kagera Sugar iliyo katika nafasi ya tatu kwenye msimamo
wa ligi hiyo itakuwa mgeni wa Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Uwanja
wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam na wenye uwezo wa kuchukua
watazamaji 7,000 uko tayari kwa mechi kati ya JKT Ruvu na Tanzania Prisons.
Nayo Ruvu Shooting itakuwa nyumbani kwenye uwanja wake Mabatini ulioko
Mlandizi, Pwani kuikabili Oljoro JKT kutoka Arusha.
0 COMMENTS:
Post a Comment