April 10, 2013



Pamoja na kupokea mshahara wa pauni 250,000 (zaidi ya Sh milioni 625) kwa wiki, mshambuliaji wa Manchester United aliwashangaza watu leo baada ya kukutwa akiwa amekomaa kwenye mashine ya kutolea fedha maarufu kama ATM. 

Kwa watu waliokuwa eneo hilo kilionekana ni kama si kitu cha kawaida kwa nyota huyo wa Manchester United kupambana na ATM ili kupata pauni kadhaa.

Rooney akiwa amevalia suruali nyeusi na  koti maalum lenye kofia ya kuziba uso wake alionekana akiwa mtulivu pembeni mwa Coleen ambaye alikuwa anasumbuka na ATM.

Mkononi wawili hao walikuwa na mifuko ya nylon hali iliyoonyesha walikuwa wametoka katika manunuzi ingawa ilikuwa si lahisi kujua walikuwa wamenunua vitu gani.

 
Kwa fedha anazolipwa kwa wiki ukiachana na zile za matangazo, lakini bado Rooney aliongozana na mkewe na kujichimbia kwenye ATM hiyo wakichukua fedha.

Rooney na Coleen ambaye ni mjamzito walikuwa wakijaribu kutoa fedha katika ATM hiyo ambayo hairuhusu mtu kuchukua zaidi ya pauni 250 (Sh 625,000) kwa siku.

Hali hiyo imetafsiriwa kwamba Rooney aliishiwa wakati akifanya manunuzi katika eneo la Tesco katika kitongoji cha Wilmslow.

Kwa upande wake Rooney maarufu kama Wazza awali hakujua kama yeye na mkewe walikuwa wakifuatiliwa na mpigapicha wa The Sun.

Lakini baadaye alipogeuka na kugundua, alitabasamu na kumueleza kitu Coleen, halafu taratibu wakaondoka zao huku wakipiga stori na kucheka.

Pamoja waliingia katika gari la kifahari lililokuwa likiendeshwa na Coleen na kuondoka eneo hilo kwa mbwembwe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic