April 10, 2013



 
Barcelona imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya PSG kwenye Uwanja wake wa nyumbani wa Camp Now.

Barcelona ilipata sare hiyo usiku huu baada ya kusawazisha bao katika dakika ya 71 kupitia Pedro.


Wageni PSG walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 50 kupitia Pastore aliyegongeana vizuri na Ibrahimovic.

Barcelona pamoja na kuwa nyumbani walionekana hawana makali hadi alipoingia Messi aliyeanzia benchi kutokana na kuwa majeruhi.

Sare ya 2-2 jijini Paris ilifanya matokeo ya jumla kuwa 3-3 lakini Barcelona wakafuzu kwa advantage ya mabao mawili ya ugenini.

Mechi nyingine ya nusu fainali, pamoja na kuwa nyumbani, Juventus walijikutaka wakitandikwa mabao 2-0 na Wajerumani wabishi, Bayern Munich.
Bayern imekuwa timu ya pili kuingia nusu fainali kutoka Ujerumani baada ya Borussia Dortmund jana kusonga mbele dhidi ya Malaga.

Mabao ya Wajerumani hao yalifungwa na Mandzukic na mkongwe Pizzaro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic